Mchezaji mwenye umri mkubwa duniani Kazuyoshi Miura (55) bado hajataka kustaafu soka na amesaini mkataba wa mkopo na club ya Oliveirense ya daraja la pili Ureno.
Kazuyoshi Raia wa Japan anakaribia kutimiza umri wa miaka 56 mwaka huu (February 26) na anajiunga na Oliveirense akitokea Yokohama FC ya J-League.
“Japokuwa hii ni sehemu mpya kwangu mimi nitafanya kazi kwa bidii na kuonesha mimi ni aina ya mchezaji gani ambaye nimekuwa nikijulikana katika soka”>>> Miura
Miura ambay inadaiwa anataka kucheza soka hadi akiwa na miaka 60, Ureno inakuwa nchi yake ya sita kucheza soka baada ya Brazil, Japan, Italy, Croatia na Australia.
Miura alianza kucheza soka 1986 akiwa na Santos FC ya Brazil na ameandika rekodi 2017 ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kufunga katika Japanese professional league alifanya hivyo dhidi ya Thespakusatsu Gunma akiwa na miaka 50 na siku 14.