Michezo

Huyu ndio mchezaji wa Chelsea aliyesema anategemea kuondoka Chelsea kabla ya msimu mpya

on

Demba+Ba+Chelsea+v+Tottenham+Hotspur+Premier+UosTk8Q8Lc8lMshambuliaji wa Chelsea Demba Ba amefunguka na kusema maneno ambayo yanaweza kuwa mwiba kwa baadha ya wapenzi wa Chelsea.

Ba amesema kwamba kuna asilimia kubwa anaweza kuondoka Chelsea mwishoni mwa msimu, wakati akisisitiza yeye na washambuliaji wenzake wa Chelsea hawana kipya cha kuthibitisha juu ya uwezo wao kwa kocha Jose Mourinho.

Mourinho hivi karibuni alikaririwa akisema kwamba hakuwa na furaha na washambuliaji alionao, Ba mwenye miaka 28 akiwa mmoja wao.

Mshambuliaji huyo wa Senegal amebakisha miezi 12 kwenye mkataba wake wa miaka 3 na nusu aliosaini kufuatia uhamisho wake kutoka Newcastle United January  2013.

Akizungumza na RMC mshambuliaji huyo alisema anatagemea kuondoka kabla ya msimu wa 2014-15.

“Sijui kama nitakuwepo hapa, ila ninategemewa kuondoka Chelsea, ingawa bado sijafanya uamuzi wa mwisho.”

Tupia Comments