Mchezaji wa zamani wa Man City Dickson Etuhu ,37, afungiwa miaka mitano kujihisisha na soka kutokana na kubainika kuwa alihusika kupanga matokeo ya mechi May 2017.
Etuhu alihusika kupanga matokeo baada ya kubainika kuwa alimshawishi mchezaji mwenzake wa AIK Stockholm anayejulikana kwa jina la Kane Stomatopoulos kupanga matokeo katikamchezo dhidi ya Gothenburg.
Inaaminika kuwa golikipa Stomatopoulos alipewa ofa ya pauni 180,000 (Tsh milioni 520) na Etuhu ili acheze chini ya kiwango mchezo huo baada ya golikipa namba moja wa timu hiyo kuumia na kuukosa mchezo huo.
Etuhu alinakana mashitaka hayo ila baada ta uchunguzi wa kina November 2019 alibainika kufanya kosa hilo hivyo sasa chama cha soka Sweden kinamfungia miaka mitano kucheza soka ambapo adhabu hiyo itamfanya asiwe na nafasi ya kucheza soka nchi za Scandinavian hadi April 13 2025.