Top Stories

Mchungaji aliyegoma kupeleka Watoto shule akidai Mungu anazuia, ahukumiwa (video+)

on

Mahakama ya Wilaya Bukoba imemtia hatiani Mchungaji Merchades Buberwa mkazi wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera kwa makosa matatu kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili yeye pamoja na mke wake yakiwemo makosa ya Sheria ya mtoto na kushindwa kutimiza wajibu wao kama wazazi kwa kutowapeleka watoto shule.

Mchungaji huyo amehukumiwa kifungo cha miezi sita faini ya shilingi milioni moja kwa kila kosa huku mke wake akipewa kifungo cha nje na masharti ya kutotenda kosa lolote ndani ya kipindi cha miezi sita.

Akiongea nje ya Mahakama Wakili wa Serikali ameeleza kwa undani juu ya kesi hiyo.

MAMA AFANYA MAOMBI NA KULIA MAHAKAMANI BAADA YA MUME WAKE KUFUNGWA “UMENIACHA BABA,NIKUMBUKE”

 

Soma na hizi

Tupia Comments