AyoTV

VIDEO: Halima Mdee alazwa Rumande, Wakili wake kaongea

on

February 29 2016 Jeshi la Polisi Dar es salaam linamshikilia Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwa tuhuma za kufanya shambulizi la kumpiga mtu, tukio linalodaiwa kutokea siku ya February 27 wakati ilipotangazwa kuzuiliwa kwa uchaguzi wa Meya wa Dar.

Nje ya jengo la Polisi Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na Wakili wake Prof. Abdallah Safari amezungumza na AYO TV na kusema>>>‘Halima ameshitakiwa kwa kosa la shambulizi la mwili ambalo kisheria ni kosa dogo, wanasema alimshambulia RAS wakati wa uchaguzi ulipoahirishwa pale karimjee hall juzi’

‘kwa hiyo nimekuja kushuhudia maelezo yake akiandika kwa maoni yangu halima hakuhusika kabisa na hicho kitu lakini kama kawaida ya polisi wamemkatalia dhamana kwa hiyo halima atalala rumande leo’

Unaweza pia kuitazama hii Video hapa chini kuipata full stori….

Na hii ni video ya siku vurugu zilivyotokea….

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments