Top Stories

Mdundo music yaleta playlist maalum kwa ajili ya Mwezi Mtukufu

on

Kampuni maarufu ya muziki ya Mdundo Music imetangaza kuwawezesha Waumini wa dini ya kiislamu kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kusikiliza orodha maalum ya muziki wa kaswida kuanzia Aprili 1 – 30 msimu huu wa Ramadhan, kila siku ambapo mdundo.com inatoa fursa ya kipekee kwa Waumini hao kupakua mpangilio wa muziki maalum wa Kaswida kutoka kwa maDJ mbalimbali kukuza safari yao ya kiroho.

Maudhui husika yanajumuisha aina mbali za muziki ikiwemo Kaswida, Taarab, Singeli, Injili, Bongo, Naija/Afrobeat, Amapiano, Hiphop na nyingine nyingi, pia Clouds FM wameungana na mdundo.com kuwapa Wasikilizaji muziki mchanganyiko kutoka kwa MaDJ maarufu ambao sasa unapatikana kupitia ukurasa wa @mdundomusictz

Tupia Comments