Habari za Mastaa

Meek Mill amuomba Nicki Minaj msamaha kwa kumshambulia Drake Twitter… (Video).

on

drizzy meek

Kwenye headlines sasa hivi ni issue ya Meek Mill kumponda msanii mwenzake Drake kwenye mtandao wa Twitter akidai kuwa Drizzy Drake haandiki mistari yake mwenyewe na hivyo sio Mcee King.

Baada ya kumshambulia Drake kwenye Twitter, Drake nae kajibu akisema “kitu kizuri siku zote hushambuliwa hii sio issue”. Kizuri ni kwamba inaonekana Meek Mill kajishitukia kuwa alichokifanya Twitter hakijampendeza mpenzi wake Nicki Minaj.

meek

Jana rappa huyo alichukuwa time kumuomba mpenzi wake Nicki Minaj msamaha kwa kitendo alichokifanya wakiwa kwenye show yao jijini Virginia.

Akiwa on stage Meek Mill alisikika akisema: “nataka nichukue time hii kumuomba msamaha Nicki Minaj kwa kitendo cha kijinga nilichokifanya kwenye Twitter” na kwa muonekao wa Nicki Minaj… yote yameisha.

drake2

>>> “msinichukulie vibaya, kama shabiki mkubwa wa Drake nilikerekwa na kitendo cha yeye kunipa mistari ya verse ya wimbo ambayo hajaiandika… niilichokuwa nakisema ni kwamba ukilinganisha na akina Jay-Z, Nas, Biggy Smalls na 2Pac Drake sio mkali kimistari kama anavyodai”. <<< Meek Mill.

>>> “shoutout to Drake watu wangu, namkubali sana mshikaji…” <<< Meek Mill.

Nimekusogezea vipande vya video wakati Meek Mill akiwa anaomba msamaha huo mbele ya Nicki na mashabiki.

 Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments