Top Stories

Meli za mizigo zagongana

on

Meli mbili za mizigo ziligongana Kusini mwa Sweden, na kusababisha kupinduka kwa meli moja na mabaharia wawili kuzama baharini, kulingana na mamlaka ya baharini ya Sweden.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2:30 saa za kimataifa, katika Bahari ya Baltic kati ya ncha ya kusini ya Sweden na kisiwa cha Denmark cha Bornholm kati ya meli ya mizigo ya Uingereza na meli ya Denmark, ambayo ndiyo iliyopinduka, msemaji wa mamlaka hiyo, Carl- Johan Linde ameliambia shirika la habari la AFP

Watu kadhaa wanahofiwa kuwa majini na operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea, Operesheni kubwa ya uokoaji inayohusisha boti tisa na helikopta inaendelea, katika maji baridi sana, yenye digrii nne tu.

SHABIKI WA SIMBA ULAYA LEO ZIMEPIGWA PASI KAMA MILIONI HIVI

Soma na hizi

Tupia Comments