Top Stories

Membe atua kutoka Dubai “sikufuata pesa, nitue na Helikopta, majirani nawapa salam” (+video)

on

Leo September 15, 2020 Bernard Membe ambaye ni Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo amerejea kutoka Dubai na kuweka bayana msimamo wake juu ya kugombea nafasi hiyo.

“Siku 5 zilizopita niliondoka kwenda Dubai, kumekuwa na malalamiko kwamba huyu Bwana ameondoka muda huu kwanini, mimi huenda Dubai mara 4 kwa mwaka kwasababu mimi ni Mjumbe wa Bodi wa kampuni moja kubwa sana ya Dubai na tunakutana mara 4 kwa mwaka, napokwenda natumia fursa hiyo kupima afya yangu pia, nimepima nipo imara”  Membe

“Jambo jingine niseme tu kwamba mbio za Urais ni sawa na mbio za marathon ya Mita 800 unaweza ukakimbia ukaangalia nyuma ukacheka Watu lakini anayeshinda ni yule anayemaliza, mchezo wa Urais uko hivyo, mimi nimeshiriki Chaguzi 6 katika Nchi hii, nimeshiriki Chaguzi 12 katika Bara la Afrika naelewa” Membe

 

Soma na hizi

Tupia Comments