Habari za Mastaa

Cheki majibu ya staa wa movie Nigeria kwa wanaosema ‘hafuati uzazi wa mpango’… (Video)

on

Maisha ya mastaa yako kwenye macho na masikio ya watu kila wakati.. inawezekana suala la mtu kuwa na watoto wengi au kujifungua mfululizo sio kitu kigeni sana kwa sababu kwenye maisha ya kawaida watu wengi wanafanya hivyo, stori inakuwa tofauti kitu hichohicho akikifanya staa !!

Mercy Johnson ni staa wa Movie tuliyemfahamu long time kutoka Nigeria, ana watoto wawili na mtoto wake wa mwisho kujifungua ana kama miezi sita tu, na tayari ana ujauzito mwingine… hafuati uzazi wa mpango??? >>> ‘Ninatarajia kujifungua mtoto wa tatu, mimi nimeolewa na ni mtu mzima kwa hiyo watu wasiulize kwa nini… najua umuhimu wa kupishanisha muda wa kujifungua watoto, lakini nina uhuru wa kuamua kuhusu maisha yangu…

MERCY II

Kwa wale wanaoona anakosea kuwa na mtoto mwingine kwa sasa, amewajibu hivi >>> ‘Asanteni kwa wanaoniombea heri na wanaoniombea mabaya pia… ila kwa wanaotaka kuniongelea vibaya wabakize maneno mengine ya baadae kwa sababu mtoto wa nne pia atafuatia muda sio mrefu, hapo ndio mtaonesha hasira zenu ila kwa sasa tusherehekee tu hii habari njema‘>>> Mercy Johnson.

Kwenye maneno mengine amejibu haya kuhusu uigizaji wake na ishu ya watoto >>> ‘Najua itaathiri kazi yangu lakini ninachokifanya ndio uamuzi wangu niliouchagua‘– Mercy Johnson.

Mercy kayasema yote kwenye hiki kipande cha video pia mtu wangu.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments