Habari za Mastaa

Staa wa movie Nigeria amejifungua mtoto wa tatu, alivyoambiwa hafuati ‘uzazi wa mpango’?

on

Staa wa movie toka Nigeria ni staa Mercy Johnson ni moja ya mastaa ambao tuliwafahamu siku nyingi sana kwa wale watu wanaofatilia movie… kwa kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba, mrembo huyo aliwahi pia kuwa kwenye movie moja na marehemu Steven KanumbaDar 2 Lagos‘.

DAR 2 LAGOS

Niliwahi kukusogezea stori kwamba mrembo huyo ni mjamzito na stori hiyo ikaonekana kama kuna watu waliona hafatilii utaratibu wa uzazi wa mpango, kwa vile alikuwa na ujauzito wakati mtoto wake wa mwisho alikuwa na miezi sita tu wakati huo.

Majibu yake yalikuwa haya wakati ule >>> ‘Ninatarajia kujifungua mtoto wa tatu, mimi nimeolewa na ni mtu mzima kwa hiyo watu wasiulize kwa nini… najua umuhimu wa kupishanisha muda wa kujifungua watoto, lakini nina uhuru wa kuamua kuhusu maisha yangu…‘- Mercy Johnson.

Mercy-Johnson-Baby-3-1

Mercy na mume wake Prince Odi Okojie wakiwa na mtoto wao Hospitali baada ya kujifungua.

Hongera kwake mwigizaji Mercy Johnson kwa kujifungua mtoto wake wa tatu ambaye ni wa kike.

Mercy amejifungua akiwa Marekani, lakini kuna majibu mengine aliyatoa mwezi September kuhusu uzazi wa mpango >>> ‘Asanteni kwa wanaoniombea heri na wanaoniombea mabaya pia… ila kwa wanaotaka kuniongelea vibaya wabakize maneno mengine ya baadae kwa sababu mtoto wa nne pia atafuatia muda sio mrefu, hapo ndio mtaonesha hasira zenu ila kwa sasa tusherehekee tu hii habari njema..‘-  Mercy Johnson.

Video iliyobeba majibu yake yote hii hapa kuhusu uzazi wa mpango.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments