Michezo

Messi aeleza kwa nini alimjibu Abidal na tuhuma za kuiendesha Barcelona

on

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na club ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi amewatoa hofu mashabiki wa Barcelona kuwa hana mpango wa kuihama club hiyo kama inavyohofiwa, hofu hiyo ilikuwa kufuatia Messi kutoa kauli inayokinzana na Eric Abidal ambaye ni mkurugenzi wa soka FC Barcelona.

Kupishana kauli kwa Messi na Eric Abidal kunadaiwa kuwa kulikuja baada ya Abidal kufanya mahojiano na kudai kuwa wachezaji wa FC Barcelona walikuwa hawajitumi hadi wakasababisha kocha Ernesto Valverde afukuzwe kazi, kauli ambayo Messi aliijibu na kumtaka Abidal aweke wazi majina ya wachezaji hao anaodai hawajitumi kwani kutotaja jina kuna wachafua wachezaji wengi.

Leo Messi kafunguka akihojiwa na Mundo Deportivo kwa nini alimjibu Abidal kuhusiana na tuhuma hizo “Sijui nini kilimjia kichwani kwake hadi kusema vile na nilijibu kwa sababu nilihisi kama nimeshambuliwa, nilijisikia kama anawashambulia wachezaji”>>>Messi

“Kuna mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa katika vyumba vya kubadilishia nguo kwamba tunapanga kila kitu (wachezaji), tunachagua wachezaji (kuhusiana na kufukuzwa kwa kocha) kwamba mimi (Messi) nina nguvu ya kufanya maamuzi na naiendesha club hiyo sio kweli na sijui hayo maneno yanatoka wapi”>>>Messi

VIDEO: MECKY AGOMA KUMTUPIA ZIGO LA LAWAMA TINOCO KIPIGO CHA 1-0 CHA SIMBA

Soma na hizi

Tupia Comments