Michezo

Messi ajitosa kumsaidia Ronaldinho atoke rumande

on

Mchezaji nyota wa klabu ya soka ya Barcelona ya Hispania Lionel Messi ameanza mchakato wa kumtoa Rumande mchezaji nyota wa zamani wa Brazil na Barcelona Ronaldinho Gaucho.

Messi anatarajia kuwalipa mawakili Euro Milioni 4 ili kufanikisha kumtoa rumande nyota huyo wa kibrazil ambaye anashikiliwa nchini Paraguay kwa kosa la kugushi Hati ya kusafiria.

Ronaldinho na kakaye wamekamatwa na Polisi nchini Paraguay Machi 6 kwa kosa la kutumia paspoti feki kuingia nchini humo.

Mchezaji huyo alikwenda Paraguay kwa ajili ya uzinduzi wa kitabu na kampeni kuhusu watoto wanaoishi kwenye mazingira duni.

MBOWE AHUKUMIWA KWENDA JELA AU MILIONI 350, KESI YA MAUAJI YA AKWILINA HAIHUSIKI

Soma na hizi

Tupia Comments