Michezo

Messi anaandika historia Wandametropolitano

on

FC Barcelona usiku wa December 1 2019 walisafiri kutoka jiji la Barcelona hadi jiji la Madrid katika uwanja wa Wandametropolitano unaotumiwa na Atletico Madrid kama uwanja wao wa nyumbani.

Game hiyo ilikuwa ni game ya 14 ya FC Barcelona katika Ligi Kuu Hispania lakini waliingia nahodha wao Lionel Messi akiwa na rekodi mbovu katika uwanja huo, kwani alikuwa hajawahi kufunga.

Barcelona walikutana na wakati mgumu kweli kweli kiasi cha kucheza mchezo kwa dakika zaidi ya 80 bila kupata goli, jitihada binafsi za Lionel Messi dakika ya 85 ndio ziliipa uhakika Barcelona ya kuondoka na point zote tatu baada ya mchezo kumalizika 1-0.

Goli hilo linamfanya Lionel Messi kuandika historia ya kufunga goli lake la kwanza katika maisha yake ndani ya uwanja wa Wandametropolitano lakini likiwa goli lake la 30 kuwahi kuifunga Atletico Madrid aliyowahi kucheza dhidi yao katika michuano mbalimbali.

Ushindi huo inakuwa ishara nzuri kwa Barcelona ambayo inasubiri December 18 kucheza mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid, wakati huu wakiwa wamefungana kwa kuwa na point 31 wakicheza michezo 14 kila timu ila Barcelona anaongoza Ligi kwa tofauti ya goli moja dhidi ya Real Madrid.

Soma na hizi

Tupia Comments