Michezo

Isikie Kauli ya Rais wa Barcelona kuhusu hatma ya maisha ya soka ya Messi!!

on

mess

Maisha ya soka ya staa wa soka duniani Lionel Messi yalianzia katika klabu ya Barcelona tangu akiwa na miaka 13 na alilelewa hadi sasa kuweza kujulikana na kuheshikama duniani kote kutokana na kipaji chake.

Akiwa na miaka yake 27 kwa sasa alitazamiwa kuihama klabu hiyo mapema mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kutokea kutoelewana na viongozi wake wa juu lakini kauli iliyotolewa kwa sasa na Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu imemtaka Messi kubaki hadi atakapostaafu soka lake.

Maamuzi ya Rais huyo yanatokama na uwezo mkubwa na sapoti ambayo Messi amekua akiitoa ndani ya klabu yake na kusema wapo tayari kumgharamia hadi atakapoamua kuachana na soka.

Klabu mbalimbali kama Manchester United, Manchester City na hata Chelsea zimekuwa zikimuwinda sana Messi ambaye juzi alitimiza bao lake la 400 akiwa Barcelona.

millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa….  unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments