Michezo

Messi atwaa Kombe lake la kwanza na Argentina

on

Hatimae Lionel Messi anashinda Kombe lake la kwanza na Timu ya Taifa baada ya Argentina kuifunga Brazil leo goli 1-0 lililofungwa na Di Maria dakika 22 katika michuano ya Copa America.

Messi amefanikiwa kucheza fainali nne za Copa America 2007, 2015 na 2016 zote Argentina alipoteza kabla ya fainali ya nne leo kuandika historia mpya.

Messi amefanikiwa pia kuibuka mchezaji bora wa mashindano, mfungaji bora akiwa na magoli 4 na assist 5, amechangia katika magoli 9 ya Argentina kati ya 12 yaliofungwa katika michuano hii huku akicheza dakika zote 630 za michuano hiyo sawa na mechi 7.

Soma na hizi

Tupia Comments