Mix

“Messi hatojiunga na PSG au klabu yoyote hivi karibuni.” Asema Baba yake

on

360036_heroa

Lionel Messi hatoandoka  Barcelona kujiunga na Paris Saint-Germain au klabu nyingine yoyote katika kipindi cha hivi karibuni, baba na wakala wa mwanasoka huyo bora wa dunia kwa mara nne mfululizo amesema.

Matajiri wa Paris wamekuwa wakiripotiwa kuandaa ofa ya rekodi ya dunia ya kiasi cha €250 million wakati wa dirisha kubwa la usajili ili kumleta staa huyo wa Barca katika  Ligue 1.

Hata hivyo,  Jorge Messi amekanusha taarifa hizo zinazosema kwamba mwanae ataenda Paris kutoka Camp Nou na kusema Messi hatoondoka Barca hivi karibuni.

“Nimesikia kuhusu tetesi hizo na sijui wapi zinatoka,” Jorge Messi aliliambia gazeti la L’Equipe wakati alipoulizwa taarifa kuhusu PSG. 

“Hakuna chochote mpaka sasa. Lionel ni mchezaji wa Barcelona, ambapo ana mkataba kwa miaka kadhaa ijayo mpaka 2018.

“Ni heshima kujua PSG wanamfikiria yeye, lakini narudia tena hilo suala sio moja ya vitu tunafikiria kwa sasa.

“Ukweli pekee ni kwamba ana mkataba na Barca. Hatutaki kufikiria kuhusu timu nyingine aidha Paris au timu nyingine yoyote kwa sasa.”

Tupia Comments