Siku chache baada ya kutwaa Kombe la Dunia akiwa na Argentina Lionel Messi imeripotiwa kuwa amewahakikishia Viongozi wa PSG kuwa atasaini mkataba mpya.
Mtandao wa mailsports umeripoti kuwa Messi amewahakikishia kuwa ataendelea kuwepo Parc de Prince kwa msimu mmoja zaidi, licha ya kuwa kumekuwepo kwa tetesi kuwa anaweza kutimkia MLS Marekani katika timu ya Inter Miami ambayo moja ya wamiliki wake ni David Beckham.
Mkataba wa sasa wa Messi na PSG unamalizika June 2023 hivyo atakuwa Mchezaji huru kama hatoongezewa mkataba na kikanuni kwa muda uliosalia katika mkataba wake anaweza kufanya mazungumzo na club yoyote.