Kampuni ya Meta imezindua programu mpya ya motisha inayoitwa Breakthrough Bonus, inayowapa waundaji wa maudhui (Content Creators) wa Mtandao wa TikTok hadi $5,000 (Tsh Milioni 12) kwa muda wa miezi mitatu ili kuendelea kuchapisha maudhui yao kwenye mtandao wa Instagram na Facebook.
TikTok ikiwa bado inafanya kazi kwa sasa, licha ya sheria inayopiga marufuku tovuti nchini Marekani, Meta inalenga kuwavutia waandaaji wa programu na watengeneza maudhui wa mitandao hiyo kwa “mpango mpya wa mafanikio wa bonasi.”
Ili kushinda hili, lazima uwe na umri wa zaidi ya miaka 18, unaoishi Marekani, na uwe na mtumiajia wamitandao hiyo miwili” Kiasi cha bonasi, kama unavyoweza kutarajia, kitategemea saizi ya uwepo wako kwenye mtandao mmoja wapo wa kijamii.
Pesa zitapatikana katika siku 90 za kwanza, ikizingatiwa kuwa unashiriki angalau reel 20 kwenye Facebook na 10 kwenye Instagram na machapisho lazima yafanyike kwa angalau tarehe 10 tofauti na lazima yawe maudhui asili.
Mpango huu ni sehemu ya mkakati mpana wa Meta wa kuvutia waundaji wa TikTok na kupanua mfumo wake wa video fupi fupi, haswa wakati TikTok inakabiliwa na sakata la kufungiwa nchini Marekani.