Mstahiki meya Wa Jiji la Arusha mh Maximilian Iranghe ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano Wa Mameya Wa Majiji yote yenye nguvu Duniani (Strong City network) Mkutano uliofanyika Nchini Marekani Katika Jiji la New York
Mkutano huo ulioanza Sept 21 nimkutano Muhimu unaojadili Maswala Mbalimbali ya maendeleo ya miji pia ulijadili namna mameya wanavyoshiriki kukabiliana na chuki, siasa kali, mpasuko wa kimaadili yaani.
Pamoja na Utunzaji Wa Mazingira moja kati ya Mafanikio Tanzania iliyofanikiwa kuipata kutokana na Mkutano huo hadi hivi Sasa ni Tanzania imenufaika Kwa kukubaliwa kuandaa Mkutano mkubwa Wa Mameya Wa Majiji yote ya Afrika mwaka 2024 baada ya ushawishi uliofanywa na Meya Maximilian kuletwa Kwa Mkutano huo Nchini Tanzania na Moja kati ya sifa alizozieleza Meya Maximilian Iranghe katika Mkutano huo wakati akipigia chapuo nchi ya Tanzania kuandaa Mkutano huo alieleza juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika utunzaji Wa Mazingira akigusia Uwepo Wa hifadhi nyingi za Taifa na Mapori tengefu ambazo nikielelezo kuwa kama nchi inafanya juhudi kubwa ya kuhifadhi Mazingira kupitia Misitu,lakini Uwepo Wa kampeni ya kupanda miti 1,500,000 jijini Arusha huku kukiwa na miti zaidi ya elfu mbili iliyopandwa Kwa muda Wa mwaka Moja Hadi hivi Sasa.
Sababu hizo pamoja na za utulivu Wa kisiasa chini ya usimamizi Wa Rais Mwanamke Mh Dkt Samia Suluhu Hasani zinaelezwa kuwa ni Miongoni mwa sababu ziliiwezesha Tanzania kupata Nafasi hiyo ya kuandaa Mkutano huo.
Meya Eric Adam ni Miongoni mwa Mameya watano wenye nguvu Duniani kwenye Maswala ya Siasa, Katika Mazungumzo Yao Mstahiki meya Maximilian Iranghe amemuaalika Meya huyo kuhudhuria pia katika Mkutano huo Mkubwa Wa Wa Mameya Wa Afrika unaotarajiwa kufanyika mwakani Nchini Tanzania na kumpatia zawadi ya kofia yenye nembo ya Mlima Kilimanjaro.Mh Maximilian ameeleza kuwa kufanikiwa kushawishi Mkutano huo Mkubwa Wa kimataifa kuja Nchini Tanzania kutafungua fursa zaidi kwenye Maswala ya Utalii na ukuongeza Pato la nchi Kwa kuwa wageni wote watakaokuja Tanzania Kwa nmna Moja au nyingine watanunua bidhaa,watalala na kula kwenye Mahotel ,watatembelea hifadhi zetu za Taifa na kuongeza mzunguko Wa fedha za kigeni.