Meya wa zamani wa Ubungo, Bonifave Jacob amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akisema ameingia kama mahabusu lakini ametoka akiwa Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani kupitia CHADEMA.
Jacob ambaye ameachiwa kwa dhamana baada ya kusota mahabusu kwa takribani siku 20 amewaambia Waandishi wa Habari kwamba amejifunza mengi gerezani hadi kufikia hatua ya kuanza mchakato wa kuwasaidia wafungwa 10 kwa kuwalipia faini, huku washtakiwa 20 atawapatia msaada wa kisheria ikiwemo kuwapa Mawakili.
Jacob anakabiliwa na mashtaka mawili katika mahakama hiyo ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, uamuzi wa dhamana umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga ambaye ameahirisha kesi hiyo hadi October 21,2024.