Habari za Mastaa

Kuhusu msanii Mez B kuchomwa kisu

on

mez bMsanii wa Chemba Squad Mez B Jumamosi iliyopita amechomwa kisu na watu asi0wafahamu maeneo ya Sinza karibu na Vatican City Dar es salaam katika kisa ambacho bado mpaka sasa kina maswali mengi juu yake.

Anasema ‘ilikua Sinza niliagizia chakula na kuagiza kinywaji nikawa nimekaa lakini ghafla akaja mtu akawa anatukana kila kitu nikiwemo mimi na Serikali alafu baadae nikawa naona anaongea na Mabaunsa kisha wakati naondoka yule baunsa mmoja akanivuta akaniambia haiwezekani huyu akutukane hivyo hebu ngoja nimuulize, ndio akamwambia yule jamaa >> ebwana we fanya kazi yako’

‘Ndio akaanza kunichana na kisu, nia yake ilikua kuniua na wale Mabaunsa walikua wanaangali tu, nimeumia sana kwa michano ambapo Madaktari wameniambia hakuna haja ya kushona, nimevuja sana damu…. nilipata matibabu usiku uleule baada ya kuripoti Polisi Mabatini’

Mez B ameyasema hayo kwenye interview na Doreen Andrew wa XXL Clouds FM, unaweza kumsikiliza hapa chini

Tupia Comments