Habari za Mastaa

Picha za kwanza zinazomuonyesha msanii Mez B jinsi alivyochomwa visu na mtu asiejulikana.

on

2Taarifa za msanii Mez B kushambuliwa na mtu asiemfahamu wala kuwa na ugomvi nae usiku wa Jumamosi akiwa maeneo ya Sinza ni miongoni mwa stori zilizosambaa sana toka jana.

Mez B kwenye interview fupi na millardayo.com amesema amepata majeraha mengi maeneo ya usoni na anasema kwamba kuna kisu alikikwepa kikielekezwa shingoni wakati aliporushiwa visu mbele ya Mabaunsa wa sehemu ya burudani Sinza waliokua wakishuhudia bila kutoa msaada wowote.

Mez B tayari ameshaifikisha hii ishu kwenye vyombo vya sheria ili kila kitu kikae kwenye mstari kuhusu mtu huyu aliemshambulia ambae Mez anadai alimkuta mahali anasubiria kufungiwa chips zake ndio akaanza kutukana watu mbalimbali ikiwemo Serikali na Mez B mwenyewe.

Baada ya hapo wakati Mezi akiondoka, baunsa mmoja kwenye eneo hilo alimwita na kumwambia haiwezekani huyu jamaa akutukane hivihivi hebu njoo tumuulize, tofauti na alivyotarajia… Mez anasema yule Baunsa ndio alimfata yule mchoma visu na kumwambia amalize kazi, yani akamshambulie Mez B.
1

3
4
5
6

Tupia Comments