July 25, 2018 KCB Bank Tanzania imeendelea kuonyesha dhamira ya kuwaendeleza wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) kwa kuendesha kongamano la pili kwa wafanyabiashara zaidi ya 200 jijini DSM.
KCB Bank wameanzisha Biashara Club ambao ni mpango maalum ndani ya KCB Bank Tanzania unaowasaidia wafanyabiashara kukuza ujuzi katika maswala ya fedha, uendeshaji wa biashara na kanuni na misingi ya kulipa kodi pamoja na kuwapa fursa za kukuza mahusiano yao na wafanyabiashara wengine ndani na nje ya nchi.
Semina hii inayoratibiwa na KCB Bank lilizinduliwa mwaka 2017, ambapo ilitoa mafunzo ya kutunza fedha, uwekaji wa kumbukumbu za hesabu , ukaguzi wa taarifa za fedha za biashara na upatikanaji na matumizi ya wa taarifa hizo.
Semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Serena ilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani, uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo.
Nia kubwa na KCB Bank ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba.
Akiongea katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Cosmas Kimario, alisema “Hakuna biashara inayofanikiwa bila changamoto. Hizi zipo ili zikupe chachu, uzikabili, usonge mbele. Wanaokimbia changamoto huanguka kibiashara ama huendesha biashara zisizo endelevu.”
Nae Charles Adolf kutoka Adolf Tax Consultants, wataalam wa maswala ya kodi walioalikwa na KCB Bank Tanzania kutoa mafunzo katika warsha hiyo pia alipata nafasi ya kuongea na wafanya biashara hao.
Adolf aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muhimu wa kuelewa mfumo wa kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara biashara zao. “Hamna taifa linaloendelea bila kodi lakini pia ili kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi imara ni lazima tulipe kodi.”
Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua wigo wa biashara zao.
KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.
Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki.
Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar.
Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro. Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake
Weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.V
LIVE MAGAZETI: Ufisadi wa kutisha NIDA, CHADEMA waamsha upya kifo cha Akwilina