Top Stories

Mfahamu dereva wa ndugu abiria anae-trend mtandaoni afunguka

on

Leo Ayo TV inakukutanisha na Waubani Mohamedi Linyama maarufu Ndugu Abiria ambae memes zenye picha yake zimetrend sana mitandaoni.

Umaarufu alioupata kwa muda mfupi kwake una simulizi nyingi zenye raha na karaha, miongoni mwa ambayo anakiri yanamkera ni Memes zenye maneno “Ndugu abiria naenda kuwamwaga’ maana anadai zinamchafua , lakini pia zile Memes zinazosema “Ndugu abiria nina stress za Mapenzi nitawamwaga” anasema zinamletea shida kwa Mke wake ambaye huhoji hizo stress za Mapenzi anazitolea wapi?.

Kingine ambacho hakimfurahishi ni kitendo cha Kampuni mbalimbali kutengeneza Memes zenye picha yake bila kumlipa pesa na anasema tayari Kampuni kadhaa ameanza kuzifuatilia ili azifikishe kwenye mikono ya sheria ikiwemo kampuni moja ya Bima ambayo anasema wakitaka wayamalize wamlipe Milioni 200.

MFAHAMU DEREVA WA NDUGU ABIRIA ANAE-TREND MTANDAONI, AFUNGUKA “MKE WANGU HAPENDI, NILIPWE MIL.200”

Soma na hizi

Tupia Comments