Michezo

Mfahamu ‘Handsome boy’ wa EPL.

on

259187B300000578-0-image-a-4_1423658741197

 

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud ametajwa kuwa mchezaji mwenye mvuto kuliko wote wanaocheza kwenye ligi ya England katika utafiti uliofanywa miongoni mwa mashabiki hususan wa kike nchini England .

Utafiti huu ulihusisha jumla ya wanawake 250 raia wa Marekani ambao waliulizwa maswali juu ya wachezaji wanaodhani wana mvuto wa kimapenzi nchini England na utafiti huo ulimuonyesha nyota huyu Mfaransa kuwa na mvuto kuliko wote .

Wakati alipoarifiwa juu ya kutwaa tuzo hii isiyo rasmi ya mchezaji mwenye mvuto wa kimapenzi kuliko wote , Olivier Giroud alipewa zawadi ya kioo cha dhahabu na hakusita kuwashukuru wazazi wake wawili kwa kumzaa na kumfanya kuwa na mvuto huu ambao leo umekubalika kuwa bora kuliko wachezaji wote kwenye ligi ya England .

2591873200000578-0-image-a-5_1423658746412

Giroud pia aliwashukuru watu wengine kama kinyozi wake , mtaalamu wake wa masuala ya make-up, mbunifu wake wa mitindo pamoja na msaidiz wake wa masuala ya picha watu ambao kijumla wanatengeneza timu inayiomfanya aonekane kuwa na mvuto huu alio nao .

Giroud hakuwa mwenyewe kwenye utafiti huu na kuna wachezaji wengine waliotambuliwa kuwa na mvuto akiwemo mchezaji wa Sunderland Santago Vergini ambaye alishika nafasi ya pili  na nyota wa Leicester City Matty James ambaye alishika nafasi ya tatu .

Tupia Comments