Said Ntibanzonkiza ni mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Vitalo ya Burundi kabla ya jana Yanga SC kutangaza kumsajili kwa mkataba wa miezi 18.
Ntibazonkiza alizaliwa Mei 1 1987 Bujumbura Burundi na kuanza soka lake katika klabu ya VITAL’O akiwa bado mdogo.
Mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 alianza kuichezea timu ya wakubwa ya VITAL’O na kudumu hadi 2005 kisha akaanza safari ya kucheza soka Ulaya kwa kujiunga na klabu ya NEC ya Uholanzi na kudumu kwa miaka minne kuanzia 2006 hadi 2010 kisha akahamia Poland katika club ya KS Cracovia na kucheza kwa miaka minne tena akicheza mechi 85 na kufunga magoli yapatayo 17.
Upepo ukabadilika 2014 alipoanza kucheza Ligi Kuu Uturuki katika klabu ya Akshir alidumu kwa mwaka mmoja tu klabu ya Caen ya Ufaransa ikamuona na mwaka 2015 akaanza kucheza timu B na baadae timu ya wakubwa na kukipiga katika Ligi Kuu Ufaransa ambako alicheza mechi 14 na kufunga goli moja.
Safari ya soka haikuishia hapo kwa Ntibazonkiza, 2017 akahitimisha safari yake ya miaka 12 ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya kwa kuitumikia FC Kaisar ya Kazakhstan iliyopo Centray Asia kisha kurejea Burundi.
Uzoefu wake alioupata na bao zuri aliloifunga timu ya taifa ya Tanzania katika mchezo dhidi ya Burundi vilichochea viongozi wa Yanga kuamini kuwa ana uwezo wa kuisaidia timu yao.