Mfahamu Odion Jude Ighalo amerejea tena EPL kutimiza ndoto yake ya utotoni ya kucheza ManUnited kwa sasa yupo kwa mkopo wa miezi 6 akitoka China.
.
Ighalo amezaliwa 16/6/ 1989 Lagos Nigeria eneo la Ajegunle, eneo hili linajulikana kama Ghetto Kings ni hatari kwa makuzi ya mtoto japokuwa limetoa mastaa wengi sana wa muziki lakini ni eneo la watu wa chini.
Baba mzazi wa Ighalo alikuwa hana ajira rasmi wakati mama yake alikuwa akifanya biashara ya kuuza bidhaa ndogo ndogo za dukani kama vinywaji kwa Tanzania tunasema anauza duka lakini mama Ighalo pia alikuwa akitembeza na kuuza maji barabarani kama tuonavyo kwa vijana wengine Tanzania na kutunza pesa kisha kumnunulia mwanae Ighalo viatu vya kuchezea mpira.
Hili ni tatizo kubwa kwa familia nyingi sana Afrika kutamani kuwachagulia fani watoto wao na sio kusapoti wavitakavyo watoto, Mzee Ighalo alikuwa mpambanaji
alikuwa akitamani sana mwanae atie nguvu shule kuliko mpira akiamini ndio njia pekee ya kumkomboa kijana wake wakati mama alikuwa akimsapoti kimya kimya kwa kutunza pesa na kumnunulia viatu vya kuchezea mpira.
Enzi za utoto Ighalo na wachezaji wenzake wakiwa mazoezi walilazimika kulala chini kwa hofu kama njia ya haraka ya kujiokoa maisha yao kufuatia kusikika milindimo ya risasi katika uwanja wao wa mazoezi maeneo ya Ajegunle ambapo waliamini risasi zilizokuwa zinapigwa na Polisi kwa lengo la kukamata wauza dawa za kulevya haziwezi kujua huyu ni mchezaji soka mtoto na huyu ni muuza dawa za kulevya kutokana na eneo walilokuwa wanafanyia mazoezi lilikuwa limezungukwa na wahuni hii ndio sababu pia baba mzazi alikuwa akigoma mwanae kucheze soka.
Hayo ni maisha ya kawaida sana kusikia milio ya risasi kwa kijana aliyekulia Ajegunle Ghetto ni kawaida Polisi kupiga Patrol wakati wote eneo hilo sio ajabu kuona vijana wakikamatwa kila leo eneo hilo kutokana na kuwa ni eneo lililokuwa na uhuni wa aina zote usio ruhusiwa kisheria.
Kwa sasa Ighalo ni moja kati ya wachezaji matajiri Afrika, hiyo ni sehemu fupi ya historia yake ya utotoni kabla ya kuanza kupata mafanikio na vilabu mbalimbali Ulaya na Asia kama Udinese, Granada, Watford, Shanghai Greenland na sasa Man United.