Mfalme wa Uingereza Charles III anaanza ziara yake ya kwanza nchini Kenya siku ya Jumanne, akiwa na mwelekeo mkubwa wa hisia, kama mfalme katika nchi ya Jumuiya ya Madola, wakati ambapo taasisi hii inaonekana kudhoofika na wakati wito unaongezeka kwa Uingereza kukabiliana na ukoloni wake wa zamani.
Kenya inahusishwa hasa na historia ya familia ya kifalme: ni hapo mwaka wa 1952, Elizabeth II alipopata habari kuhusu kifo cha babake, Mfalme George VI, na kumfanya kuwa Malkia mpya wa Uingereza. Ziara ya Charles III na Malkia Camilla itafanyika wiki chache kabla ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wake, uliyotangazwa Desemba 12, 1963.
Mfalme Charles III na Malkia Camilla watapokelewa na rais William Ruto katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne,kwa siku mbili, watakutana kwa mazungumzo na wajasiriamali na vijana, watashiriki karamu ya serikali, watembelee jumba jipya la makumbusho linalohusu historia ya Kenya na kuweka shada la maua kwenye kaburi la askari asiyejulikana katika bustani ya Uhuru.
Kisha, Charles na Camilla wataenda Mombasa, kusini mwa nchi, ambako mfalme, anayehusika na masuala ya mazingira, atatembelea hifadhi ya asili na kukutana na wawakilishi wa dini mbalimbali.
Baada ya kuonyesha nia ya London ya kukaribiana na washirika wake wa Ulaya na ziara zake za serikali nchini Ujerumani na Ufaransa, Charles III, kwenye kiti cha enzi kwa zaidi ya mwaka mmoja, anazindua “dhamira yake ya kuokoa Jumuiya ya Madola” nchini Kenya. “, Gazeti la kila siku la Daily Mail limeripoti.