Top Stories

Mfanyabiashara amchinja Mwanae wa kiume Nigeria

on

Mfanyabiashara Mkubwa Jimbo la Zamfara nchini Nigeria amekamwatwa kwa kosa la kuua kwa kumchinja mtoto wa kiume wa miaka tisa.

Aminu Baba ambae anafanya biashara ya kuuza magari amekiri kumuua na kumchinja mtoto Ahmad Yakubu Aliyu, na kutoa baadhi ya viungo vyake ikiwemo macho na utumbo kabla ya kuutupa mwili wake.

Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Zamfara Bwana Ayuba Elkanah ameeleza kwamba mtuhumiwa amekiri kwamba amekuwa akiwaua na kuwachinja watu ikiwemo watoto na kutoa baadhi ya viungo vyao.

Mtuhumiwa Bwana Aminu amesema amekuwa akila hivi viungo na kuuza vingine kwa wengine wanaohitaji.

Mtoto Ahmad alitoweka wiki mbili zilizopita akiwa anatoka Shule ya Islamiyya alipokuwa anasoma na baadaye mwili wake ulipatikana akiwa ameuawa na kuchinjwa kinyama.

BABA ABAKA MTOTO WAKE WA KUMZAA “NI MWANAFUNZI DARASA LA 7”

Soma na hizi

Tupia Comments