Ni April 1, 2023 ambapo Millardayo.com & Ayo TV inakukunisha na stori ya Mfugaji Flavian Mbara ambae ni Mkazi wa Njombe.
Ambae amefunguka yale tusiyoyajua kuhusu Ufugaji wake mpaka namna alivyopata faida alipoanza kufanya kazi na Kampuni ya Asas.
‘Nimejiunga na Asas, kwasasa nakamua ngombe sita ambao kwa wastani Asubuhi na Jioni nauza Maziwa lita 86 hadi 100 na nachukua nafasi hii kumshukuru sana Mkurugenzi wetu wa Kampuni ya Asas Ahmed kwani ametukumbuka sisi wafugaji kwani amekuwa msaada mkubwa sana’- Mfugaji
‘Ukiona Asas amekukubali Mfugaji hadi kuchukua maziwa yako basi jua wewe ni wa viwango vya juu katika Ufugaji na soko letu linaenda vizuri na katika malipo yapo vizuri na wala hatujawahi kupitilizwa malipo kulipwa hatujawahi kufanya jambo lolote ambalo si rafiki na biashara’- Mfugaji
‘Biashara yetu inaenda vizuri watu tumefanikiwa kusomesha na kama hauna watoto basi biashara yetu inatusaidia kujenga nyumba katika makazi yetu, soko letu tulijiunganisha kama Chama cha msikamano kwahiyo Maziwa yanakusanywa katika chama cha ushirika baada ya hapo yanaenda kwa mnunuzi ambae ni Asas’- Mfugaji
‘Kwasasa nasomesha wangu kupitia Ufugaji kiukweli Asas ni mkombozi wetu kwani leo hii Maziwa ningekuwa namuuzia nani ila Asas namshukuru kwanipa hii tenda Mungu awabariki sana Asas’- Mfugaji