Godfrey Magila ni mtaalamu wa Teknolojia kwenye upande wa mitandao na ndio aliyetengeneza App ya Tigo Back-Up, amekaa kwenye Interview na Millard Ayo na kueleza urahisi wa kukamatwa kwa yeyote anaefanya kosa la kimtandao ikiwa tayari sheria ya makosa ya kimtandao imeshaanza kufanya kazi Tanzania.
Tayari watu kadhaa wameshafikishwa Mahakamani Tanzania akiwemo aliyemtukana Rais Magufuli, aliyeandika habari za uongo za mkuu wa majeshi kulishwa sumu…… wengi wanaamini sio rahisi kukamatwa hata ukitumia jina ambalo sio lako kwenye mtandao ila Magila anasema ni rahisi sana.
Anasema ‘Kila mtu aliyejiunga kwenye mtandao kuna kama unaacha alama ya unyayo kwahiyo hilo watu wanalichukulia kirahisi lakini lina umuhimu wake na ndio linafanya ijulikane muda, sehemu na taarifa nyingine kuhusu wewe pale unapotafutwa, unyayo unaonyesha mpaka aina ya simu‘
Kubadilisha jina na kumtukana mtu kwenye mtandao itasaidia usikamatwe? >>> ‘Kuna baadhi ya vitu hata ukibadilisha jina haisaidii mfano mitandao mingi ukijiunga au email unaambiwa uingize namba ya simu kwa ajili ya uthibitisho, utatumiwa msg kwenye simu ili uthibitishe…. tayari namba yako uliyoiweka ina taarifa zako nyingi na hiyo ni moja tu ya njia nyingi zinazoweza kufanya ukamatwe’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE