Leo August 2, 2018, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeziunganisha Benki ya Tanzania Women’s Bank PLC (TWB) na Tandahimba Community Bank na Kilimanjaro Cooperative Bank kuwa Benki moja kuanzia August 3, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Professa Florens Luoga amesema muunganiko wa benki hizo utaunda jina la ‘TPB Bank PLC’ kwa lengo la kuongezea nguvu Benki hizo ikiwa ni moja ya matakwa ya wanahisa wa TWB na TPB hivyo madeni ya wateja wa Benki hizo yataunganishwa kwa pamoja.
“Bank hizi zilipewa muda ili kufikisha kiwango cha mtaji kinachohitajika na sheria ya mabenki na taasisi za kifedha ya 2006 na kanuni zake cha kiwango cha chini cha Bilioni 2 kwa benki za wananchi (Community Banks)” Gavana Luoga
Luoga amesema benki hizo pia ziliongezewa muda wa mwezi mmoja hadi kufikia July 31, 2018 kufanya taratibu za kuongeza mtaji baada ya hapo wanahisa wakaamua kuzionganisha ili kuziongeze nguvu.
Aidha BOT imetangaza pia kuchukua usimamizi wa shughuli zote zilizokuwa zinafanywa na Bank M kuanzia leo August 2.
Uamuzi huo unaelezwa ni kutokana na Bank M kupungukiwa fedha za kujiendesha na kushindwa kufikia malengo yake