Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Rais Magufuli leo September 11 ameteua Wenyeviti wawili

on

Leo September 11, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. John Stanslaus Ndunguru kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Ndunguru umeanza tarehe 09 Septemba, 2019.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Prof. Antony Manoni Mshandete kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).

Prof. Mshandete ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ubunifu), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kilichopo Mkoani Arusha.

NAPE ATINGA KWA MIGUU IKULU KUOMBA ASAMEHEWE “SINA AMANI, NAKOSA USINGIZI “

 

Soma na hizi

Tupia Comments