Leo January 19, 2018 President Dr. John Pombe Magufuli amewaagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasliano Prof. Makame Mbarawa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Karume kusitisha usajili wa meli mpya nchini mpaka itakapotangazwa vinginevyo.
President Magufuli ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere, kikao ambacho kimehudhuriwa na Mawaziri hao.
JPM amewaagiza Mawaziri hao pamoja na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kwa meli zote 470 ambazo zimesajiliwa hapa nchini na zinapeperusha bendera ya Tanzania.
Namnukuu JPM >>>“Kafanyeni uchunguzi wa kina kwa meli zote zinazopeperusha bendera ya Tanzania, fanyeni uchunguzi kwa meli zilizokamatwa ambazo ni 5 na pia hizi 470 zilizosajiliwa na zinazoendelea kufanya kazi, hatuwezi kuacha jina la nchi yetu lichafuliwe na watu wanaofanya mambo kwa maslahi yao” .
President JPM amesema maagizo yote yaliyotolewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu kuhusiana na meli hizo yatekelezwe.
Pia President JPM amemuagiza Waziri Mahiga kuhakikisha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na Wakurugenzi wa idara za wizara hiyo kufanya kazi zenye manufaa kwa nchi, ikiwemo kuwataka Mabalozi kutoa taarifa kila baada ya robo mwaka juu ya ukusanyaji wa mapato.
“Wakupe taarifa kila baada ya robo mwaka, na Balozi ambaye atakuwa hakusanyi mapato vizuri na kuinua biashara na uwekezaji atakuwa hafai kuendelea kuwa Balozi, tena kawaambie kabisa kwenye suala hili hakuna mchezo” – Rais Magufuli.
JPM amewataka watendaji wa wizara ya Mambo ya Nje kufuatilia kwa ukaribu na kushirikiana na Mawaziri wanaohusika katika utekelezaji wa mikataba ambayo Tanzania imetiliana saini na nchi nyingine na kwamba hataki kusikia utekelezaji wa mikataba ya miradi mikubwa unakwama au kusuasua
“Mnapokuwa mnahitaji taarifa kutoka wizara nyingine kama ni Waziri muandikie Waziri mwenzako, Katibu Mkuu muandikie Katibu Mkuu mwenzako nakala ya barua ilete kwangu kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, nataka nione atakayechelewesha ama kutotoa taarifa” -Rais Magufuli.
GARI YA FFU IMEPINDUKA KUTOKANA NA MWENDOKASI IMEUA ASKARI 2, KAMANDA MPINGA AMEONGEA