AyoTV

TREND ZA WIKI: Ya Rais Magufuli kuongelea kushikana mkono na Lowassa imo (VIDEO)

on

Katika zile picha zilizo-trend wiki hii ni pamoja na zile picha za Rais Magufuli na Edward Lowassa kukutana na kusalimiana kwa mara ya kwanza toka kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 ambapo wawili hawa walikua ndio washindani wakubwa.

Rais Magufuli alisemaKatika siku hii ya kuadhimisha miaka 50 ya ndoa ya Rais mstaafu Mkapa na mimi nimepata muujiza wa tofauti leo sababu ndio nimeshikana mkono na Mh. Lowassa, tumezunguka kampeni zote sikuwahi kukutana nae, nikiri kweli tulikua na ushindani mkubwa

Katika fundisho la leo nyinyi ni madhehebu tofauti huyu Lutheran mwingine Catholic lakini mmeishi miaka 50 na nina uhakika mtaendelea kuishi miaka yote iliyobaki, ni ndoa nyingi zimevunjika kabla hazijafika miaka 50, hili ni fundisho kubwa kwa sisi Wanasiasa kuwa tunaweza kuishi kwa pamoja kwa upendo hata kama ni vyama tofauti’Rais Magufuli

UMEIKOSA HII YA MAGUFULI? WANALALAMIKA PESA ZIMEPOTEA, HII MSG IWAENDEE CLEAR, TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI….

Soma na hizi

Tupia Comments