Top Stories

Rais Magufuli aagiza Mkurugenzi alietumbuliwa na Bodi arudi kazini

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati kumrejesha kazini mara moja aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio.

Katika agizo hilo, Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Nishati kumrejesha Dkt. Mataragio katika nafasi yake ya Mkurugenzi Mkuu wa TPDC ili aendelee na majukumu yake.

Dkt. Mataragio alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC tarehe 20 Agosti, 2016.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 22 Julai, 2019.

MSTAAFU MWINYI AFUNGUKA PICHA ALIYOIPOST MAKAMBA “KWA KWELI SIKUIPENDA”

Soma na hizi

Tupia Comments