Top Stories

Rais Magufuli “Kasimu kangu kimeo, kata hela popote wala sikuombi” (+video)

on

Rais Magufuli amemua kumpigia Waziri Maji simu akiwa njiani kutoka Kagera akielekea Chato ambapo amemuagiza Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ambaye yupo ziarani Mkoani Kagera kushughulikia haraka iwezekanavyo tatizo la maji katika Mkoa huo

Pia Rais amemtaka katika Kata ya Kyaka kuwa Wizara iwapeleke watalaamu watakaoweka miundombinu ya kuvuta maji ya Mto Kagera na kuyapandisha hadi kwenye mlima uliopigwa bomu wakati wa vita vya Kagera na kisha kuyasambaza kwa wananchi kwa mtiririko.

Katika maelezo yake, Prof. Mbarawa amesema Wizara itatatua matatizo ya maji katika maeneo hayo kwa kutumia fedha za Mfuko wa Maji lakini kwa Mji wa Muleba tayari Serikali imetenga shilingi Milioni 400 na Nyakabango shilingi Milioni 600 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji.

“VIJANA WANA-POST WAPO TAYARI KUMWAGA DAMU, MCHANJE NA KIWEMBE UONE”

Soma na hizi

Tupia Comments