fB insta twitter

Mgodi mwingine wa dhahabu kujengwa kanda ya ziwa

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii kwenye gazeti la Majira yenye kichwa cha habari ‘Mgodi mwingine wa dhahabu kujengwa Sengerema’ 

Gazeti hilo limeripoti kuwa mgodi mwingine wa dhahabu unatarajiwa kufunguliwa katika kijiji cha Sota, kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani Mwanza baada ya kampuni ya OreCorp Tanzania Ltd kwa kushirikiana na ile ya ACACIA kukamilisha utafiti wake kijijini humo.

Mgodi huo utatumia bilioni 30.8 kukiwa na hazina ya wakia milioni 2.8 za dhahabu, ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwakani, jambo ambalo limeelezwa litasaidia kuinua uchumi wa wananchi waishio wilayanin humo na taifa kwa ujumla.

Meneja utafiti wa Kampuni hiyo amesema kuwa utafiti huo ulianza mwaka 1999, lakini ulichelewa kuanza kutokana na kampuni kupokezana umiliki, ambapo wao wameingia ubia na kuanza kazi hapo tangu oktober mwaka jana na wanatarajia kukamilisha utafiti wa mwisho mwaka 2017.

Amesema mgodi huo utajengwa mara baada ya kuridhika kuwa matokeo ya utafiti ya waliowatangulia ya kuwepo kwa akiba ya wakili milioni 2.8 ya dhahabu katika eneo hilo yatakuwa sahihi.

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 13 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments