Top Stories

Mgombea Ubunge anaefanya kampeni kwa baiskeli alia ukata

on

Mgombea ubunge Jimbo la Musoma Mkoani Mara kupitia chama cha, ADC, Ernest Ojung’a amesema anakabiliwa na ukata wa fedha ya kuendeshea kampeni jambo ambalo linamlazimu kuomba wananchi michango.

Mgombea huyo wa ubunge amesema anakabiliwa na ukosefu wa fedha za kuendeshea kampeni jambo ambalo linampa wakati mgumu wa kunadi sera zake kwa wananchi ambapo anaimani akifanikiwa kufanya kampeni wananchi wataweza kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo la Musoma.

Ojung’a  amesema  fedha hizo ambazo anaomba kwa wananchi zitamsaidia kufanya kampeni kwani amekuwa akitumia baiskeli kupita mtaa kwa mtaa.

MGOMBEA UBUNGE ANAZUNGUKA KWA BAISKELI AAHIDI KUFUTA KODI YA MAITI

 

Soma na hizi

Tupia Comments