AyoTV

VIDEO: Nje ya Mahakama kuu baada ya kesi ya Mbowe, Wema Sepetu pembeni

on

Kutoka Mahakama kuu Dar es salaam leo jioni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameongea baada ya kutoka Mahakamani kwenye kesi iliyofunguliwa na Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Mkoa DSM na Kamshna Sirro.

Tundu Lissu amewaambia Waandishi wa habari kwamba Amri ya kuzuia Freeman Mbowe asikamatwe na wala kuwekwa kizuizini na Polisi inaendelea isipokua wanaweza kumuita kwa Mahojiano ambapo pia Mahakama itatoa maamuzi March 2 2017, zaidi unaweza kumtazama Tundu Lissu hapa chini..

Pamoja na hayo, Mwigizaji Wema Sepetu alikuwepo Mahakamani hapo toka asubuhi ambapo ameonekana jioni hii akiwa pembeni ya viongozi wa CHADEMA na baadhi ya Wafuasi wa CHADEMA walionekana kumkaribishwa kwa maneno wakati akiingia kwenye gari, hii video hapa chini itakuonyesha

FULL VIDEO: Wema Sepetu pembeni ya Freeman Mbowe Mahakamani leo Dar es salaam, bonyeza hapa chini kutazama

VIDEO:Unapotangaza mtu aje Polisi saa 5 wewe ni nani?FREEMAN MBOWE…. Tazama hii video hapa chini kumuona akiongea

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments