Leo August 18, 2018 Rais Magufuli amesikiliza kero za wananchi ambapo amepiga marufuku viongozi wa halmashauri kuwanyang’anya bidhaa zao wafanyabiashara wadogo na badala yake ameagiza viongozi wote nchini kujielekeza kutatua kero zinazowakabili wananchi ikiwemo ukosefu wa soko la mazao yao.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya wananchi wa Sengerema kudai Halmashauri ya Wilaya hiyo imekuwa ikiwanyang’anya matunda aina ya nanasi wakulima na wafanyabiashara wanaouza matunda yao mjini hapo.
Amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella kufuatilia na kutatua kero hiyo.
“Nilishasema viongozi wote niliowateua mimi msisherehekee uteuzi, mtasherehekea siku mkimaliza uongozi, nataka mchape kazi, tatueni kero za wananchi na waleteeni maendeleo” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Ona Rais Magufuli alivyomuumbua Jamaa hadharani “peleka kwa DC”