Leo October 30. 2018 Mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana Tanzania, Rebeca Gyumi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Msichana Initiative ameshinda tuzo ya mwaka huu ya haki za binadamu inayotolewa na UN.
Akizungumza na AyoTV na millardayo.com Rebeca ameweka wazi kuwa kitu kilichosababisha ashinde Tuzo hiyo ni jinsi ambavyo amekuwa akipigania haki za Watoto wa kike hasa kupata elimu.
“Tuzo hii kwakweli imetupa hamasa zaidi kubwa ya kuendelea kufanya kile ambacho tumekuwa tukifanya, kama ambavyo tumekuwa tukipigania suala la ndoa za utotoni, mimba za utotoni pia kuhamasisha mabadiliko ya sheria iliyokuwa ikiruhusu watoto kuolewa chini ya miaka 18” Rebeca Gyumi
Mabasi 10 yaliyokamatwa kwa kusafirisha samaki, RC Makalla aamuru yaachiwe