Burudani

Clouds Media waweka wazi sababu za kusitishwa Tigo Fiesta DSM (+Audio)

on

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 Sebastian Maganga amezungumza na Waandishi wa Habari na kuweka wazi sababu zilizosababisha Grand Finale ya Fiesta kutoweza kufanyika leo November 24, 2018.

Maganga ameanza kwa kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kumaliza Tigo Fiesta katika Mikoa mingine salama pia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa Uongozi wa juu kwa ushirikiano waliowapatia.

“Hakika Mungu ametuweka hai hatuna budi kumshuru na vilevile Serikali, nichukue nafasi hii kwa masikitiko kutoa taarifa kwamba ile shughuli iliyotarajiwa kufanyika hapa Leaders Club, milango ilitarajiwa kufunguliwa toka Saa 12 ila haitafunguliwa tena” Sebastian Maganga

“Tigo Fiesta 2018 Vibe Kama Lotee haitafnyika tena katika Jiji la DSM ilikuwa ifike kilele usiku wa leo haitafanyika tena kuahirishwa kwake ni kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu” Sebastian Maganga

TAARIFA: FIESTA 2018 DSM ILIYOKUA IFANYIKE LEO IMEAHIRISHWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUPATA TAARIFA HII

 

Soma na hizi

Tupia Comments