Top Stories

BREAKING: Rais Magufuli aamuru Kikokotoo cha zamani kiendelee hadi 2023 (+video)

on

Rais Magufuli ametangaza kuwa kikokotoo kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya Mifuko ya Hifadhi za jamii kuunganishwa kiendelee katika kipindi cha mpito hadi mwaka 2023, ambapo wanachama 58,000 ndio Watastaafu katika kipindi hicho.

“Nimeamua kuwe na kipindi cha mpito, nimeamua kile kikokoto kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya mifuko kuunganishwa, kiendelee kutumika katika kipindi cha mpito yaani hadi mwaka 2023” Rais Magufuli

“Kustaafu sio dhambi, Kustaafu ni heshima, huyu Mstaafu anatakiwa aheshimiwe, halafu unaanza kumpa 25% eti kwa kigezo kuwa itakusaidia kadri unavyoendelea kuishi, nani amekwambia nitaishi miaka mingapi” Rais Magufuli

 

Soma na hizi

Tupia Comments