Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi hii kuelekea Harare nchini Zimbabwe ambapo anakwenda Kumuwakilisha Rais Magufuli kwenye Sherehe za kuapishwa Rais Zimbabwe Emmerson Mnangagwa zinazofanyika leo tarehe 26 Agosti, 2018 katika uwanja wa michezo waTaifa Mjini Harare.
Akizungumza kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege Rais Mstaafu Kikwete ambaye amefuatana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Philip Mangula na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo , amesema Tanzania na Zimbabwe zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kindugu kwani katika kipindi ambacho Zimbabwe ilikuwa ikidai uhuru, baadhi ya wananchi wake waliwahi kuishi nchini Tanzania, husasani wanachama wa Chama cha ZANU PF, na kupata mafunzo hapa nchini.
‘’Baadhi ya wanajeshi wetu wameshiriki pamoja na wanajeshi wa Zimbabwe katika harakati za ukombozi wa Zimbabwe na ndio maana kwenye Jeshi letu kuna medani ya Zimbabwe’’ amesema Rais Mstaafu Kikwete.
RAIS MAGUFULI AMTUMA MSTAAFU KIKWETE ZIMBABWE, CHEYO NAE