Top Stories

Injinia amejinyonga kwa suruali, Kamanda kaongea “Marehemu aliomba rushwa” (+video)

on

Injinia wa Majego wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, Aswile Msika (37) amekutwa amekufa kwa kujinyonga katika eneo la Nyatura Kata ya Mbugani Wilayani humo kwa kutumia suruali yake.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei, amesema tukio hilo lilitokea jana ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amejitundika.

Alisema chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na Jeshi la Polisi lakini awali marehemu alikuwa na kesi ya kuomba na kupokea rushwa shauri ambalo lilikuwa linaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Chunya.

“Kabla ya tukio marehemu alikuwa na kesi ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja kutoka kwa mmoja wa wakandarasi wanaofanya kazi wilayani humo na kesi hiyo ilikuwa bado inaendelea mahakamani sasa kuhusu chanzo bado tunachunguza,” Kamanda Matei

MBUNGE ZAINABU AANZISHA VITA DHIDI MILA NA DESTURI KANDAMIZI “MWANAMKE TANGU UTOTONI ANATENGWA”

Soma na hizi

Tupia Comments