Top Stories

Viongozi Maarufu waliomzika Dada yake Rais Magufuli “Kikwete, Mwinyi, Mkapa, Odinga” na wengine (+video)

on

Leo August 21, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza Mamia ya Wakazi wa Chato katika Mazishi ya Dada yake Marehemu Monica Magufuli yaliyofanyika Chato Mkoani Geita.

Misa Takatifu ya Mazishi ya Monica Joseph Magufuli imeongozwa na Askofu Jimbo Katoliki la Rulenge Mhashamu Severine Niwemugizi aliyeambatana na Maaskofu wengine saba, pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, Marais Wastaafu Al Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dkt. Jakaya Kikwete.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula, Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi, Mawaziri, Wabunge, Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

MACHOZI: Rais Magufuli akimuongoza Mama yake kuaga Mwili wa Monica

Rais Magufuli aumizwa na maneno ya Mama yake “Bora ningetangulia Mimi Monica akabaki”

Soma na hizi

Tupia Comments