Top Stories

Mdogo wa Rostam Aziz alipa Milioni 259.5, aachiwa huru (+video)

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu mdogo wa Mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, Akram Aziz kulipa faini ya Milioni 259.5 au kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukiri mashtaka 73 ya kukutwa na nyara za Serikali ikiwemo kukutwa na nyama ya Nyati na silaha.

Hata hivyo, Akram amefanikiwa kulipa faini na kuepuka kifungo hicho cha miaka 20 jela.

Pia mahakama imetaifisha nyara hizo na kuwa mali ya serikali na kuamuru silaha zote ziwe chini ya polisi hadi hapo mshitakiwa atakapokamilisha taratibu za kisheria za kumiliki silaha hizo.

Kwa mara ya kwanza, Akram alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 31, mwaka huu akikabiliwa na mashitaka 75 katika kesi namba 82/2018 ikiwemo kukutwa na nyara za serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018 lakini kwa mujibu wa sheria alifutiwa mashitaka hayo na kusomewa upya mashitaka 73 ukitoa ya utakatishaji fedha na Meno ya Tembo.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alisema kuwa katika mashitaka ya kukutwa na nyama ya nyati, mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh 43,529,000 na katika makosa 72, yaliyobaki kila moja atatakiwa kulipa Sh. Milioni tatu.

RAIS MAGUFULI AUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MAKAMU MKUU WA CHUO CHA UDOM PROF MUBOFU

 

Soma na hizi

Tupia Comments