Top Stories

Wananchi Mbeya wamevumilia mvua ili kujisajili vitambulisho vya Taifa (picha)

on

Zoezi la uandikishaji wananchi ili kuweza kupata vitambulisho vya Taifa linaendelea katika mikoa mbalimbali nchini na moja ya mikoa iyo ni Mbeya ambapo leo January 9, 2018 Licha ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, Wananchi wameendelea kuhamasika kujitokeza kujisajili kupata Vitambulisho vya Taifa.

Afisa Usajili Wilaya ya Mbeya Alavuya Ntalima amesema katika Kata ya Ilemi zoezi limeanza Jumatano January 3, 2018 na linahusisha Kata za Iganzo, Isanga, Sisimba, Mabarini, Maendeleo pamoja na Forest.

Wakizungumzia zoezi la Usajili linaloendelea katika Kata zao Watendaji wa Serikali za vijiji wameahidi  kuendelea kushrikiana Mamlaka kuhakikisha wananchi wote wanaoishi kwenye vijiji vyao na wenye sifa wana sajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa ndani ya muda uliopangwa

Wananchi wamepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hususani la kuwatambua wananchi na kuwapatia Vitambulisho vya Taifa ambavyo vitawapa fursa ya kufanya mambo mengi na kutambulika katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulsho vya Taifa, Lodrick Hawonga, akiwapatia wananchi wa Kata ya Ilemi huduma ya Usajili kwa kuwajazia fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa.

 

BREAKING: LOWASSA AMFATA MAGUFULI IKULU

Soma na hizi

Tupia Comments